Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shabiki Simba: Tutamuunga mkono Inonga, ila mkorogo hapana!

Inonga Simba SC Henock Inonga.

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki maarufu wa Klabu ya Simba, anayefahamika kwa jina la Mchome amesema kuwa mashabiki wa timu hiyo watamsapoti beki wao Henock Inonga ambaye ametajwa kuwa 'mgeni rasmi' kwenye mchezo wao dhidi ya Jwaneng Galaxy.

Mchome amesema hayo baada ya Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally kutangaza kuwa, Jumamosi itakuwa simu maalum ya Inonga kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng utakaopigwa katika Dimba la Mkapa.

“Ishu ya mgeni rasmi, msemaji alikuja na staili ya makoti (Mgeni rasmi Kibu Denis) tukaenda kula chuma 5 kama tumesimama (mechi ya Yanga), tukaja mgeni rasmi Robertinho tukala chuma moja, leo anakuja na mgeni rasmi Inonga, staili zake imeshindikana kwenda nazo kwa sababu staili za Inonga kwa Tanzania ni haramu.

“Staili ya mkorogo, kichupa, kitaulo, umwambie mwanaume wa Dar ajichubue ni matusi. Sisi tutamsapoti mgeni rasmi Inonga kwa sababu inamheshimisha mchezaji lakini staili zako hatukuigi babu, hizo ni za kwako na Wakongo wenzako huko.

“Ishu ya kuhamasiha kwa kutumia wachezaji, Yanga ndiyo wameanzisha, sisi Simba tumekopi, sio vibaya kukopi jambo zuri kwa sababu hata wao wamekopi Yanga Day kutoka Simba Day. Maendeleo hayana chama, ukiona mtu anafanya jambo jema, ruksa kuiga,” amesema Mchome.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live