Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shabiki Simba: Hatutoboi, wachezaji wanacheza kifaza

Muha Simba Ms Shabiki Simba: Hatutoboi, wachezaji wanacheza kifaza

Wed, 6 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki wa klabu ya Simba nayejulikana kama "MUHA" Anasema kuwa bado tatizo Simba lipo kwa wachezaji, kwa sababu leo wachezaji walikuwa wakicheza kishua sana yaani ki-father zaidi.

“Bado tunalia na wachezaji, mechi ya Jwaneng wamecheza vizuri ila wanacheza kifaza. Mechi ile ilikuwa wazi kabisa, nilikuwa natembea navimba mabawa.

“Kilichoiangusha Simba ni quality ya wachezaji, tukiri tu, ukipenda mpira lazima useme kimpira. Tukiwa na mapungufu lazima tuseme, wachezaji wetu quality yao bado.

“Simba hii kufuzu robo fainali inategemeana ila kwa mpira tunaocheza ni ngumu, mpira unaonyesha unapocheza vile na timu ambazo kila nafasi wanapopata wanatumia.

“Kama tumemshindwa Jwaneng alivyo mbovu, unadhani tutashinda kwa ASEC Mimosas? Labda itokee tu lakini hatuna asilimia 100 kwamba tutashinda kwao kutokana na namna ambavyo alitupiga msako hapa. Wydad mwenyewe anataka matokeo,” amesema shabiki.

Je, ni kweli wachezaji wa Simba wanacheza Ki-Father?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live