Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shabiki Simba: Bao la Guede lina thamani ya sh bilioni 5

Guede Yanga Ms.jpeg Shabiki Simba: Bao la Guede lina thamani ya sh bilioni 5

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki maarufu wa Klabu ya Simba, anayefahamika kwa jina la Mchome amesema kuwa bao aalilofunga mshambuliaji mpya wa Yanga SC, Gnadou Joseph Guede dhidi ya CR Belouizdad lilikuwa bao muhimu la kuwacusha kwenda robo fainali.

Guede alifunga bao hilo la mwisho dakika ya 84 kwenye ushindi wa mabao 4-0 waliofunga Yanga katika Dimba la Mkapa na kuandika rekodi walioikosa kwa zaidi miaka zaidi ya 50.

“Goli alilofunga Joseph Guede dhidi ya CR Belouizdad lina thamani ya Tsh bilioni 5 kwa sababu kama asingefunga, Yanga alikuwa na kibarua kigumu mbele ya Al Ahly mchezo ujao. Na wale CR walikuwa wanatamani mechi iishe kwa sare au wafungwe goli tatu ili iwe aggregate level ya head to head halafu wao wakamuue Medeama.

“Guede wanasema anakimbia slow motion, na kawaonyesha u-slow motion kwenye kufunga. Kachukua mpira, katuliza kamwangalia kipa yuko wapi, akatia kamba na kuipeleka Yanga robo fainali. Hao ndiyo wachezaji ambao wanahitajika kwenye matukio muhimu kuibeba timu yao.

“Sio mchezaji anafunga kagoli kamoja watu wanaanza kuimba flani tusamehe… tena kwenye raundi, ya nini? Mchezaji muhimu anaibeba timu kwenye mabega yake na kuipeleka hatua ya juu zaidi, ni kama wachezaji wa Yanga. Tumemsema Joseph Guede... si huyu ameibeba Yanga mabegani?,” amesema Mchome.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live