Wakati Simba ikiwa inajipanga haswa kuhakikisha wananyalkua Kombe la Ligi Kuu msimu ujao baada ya kuwaona watani zao Yanga wakitamba kwa misimu miwili mfululizo.
Mashabiki wa Timu hiyo wameenda mbali na kudai kuwa msimu ujao sio tu watabeba makombe bali hata kiatu cha ufungaji bora kitakwenda kwa mpachika nyavu wao hatari Jean Baleke.
Akizungumza shabiki huyo wa mnyama anasema;
"Moja ya washambuliaji hatari kuwahi kuzibariki nyasi za viwanja vya Tanzania ni huyu Jean Othos Baleke.
Aliwahi kuwa mfungaji bora Congo DR mbele ya Fiston Kalala Mayele, alipo tua nchini akafanya mabalaa licha ya kuanza na timu katikati ya msimu.
Mshindani wake wa kweli ameondoka nchini naimani Jean Baleke atakuwa mfungaji bora msimu ujao kama majeraha yatamuepukia mbali"