Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Shabiki: Hersi ana akili kuliko viongozi wa Simba, Mo atuachie timu yetu

Mzee Masatu   Mzee Masatu 'Mzee wa Simba'.

Mon, 6 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki kindakindaki wa Klabu ya Simba, Mzee Masatu 'Mzee wa Simba' amesema kuwa Mwekezaji wa klabu hiyo, Mohammed Dewji anapaswa kuiachia timu hiyo ili watu wengine waendeshe timu hiyo ili ipate mafanikio zaidi.

Mzee Masatu amesema hayo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa dabi dhidi ya Yanga ambapo Simba ilikubali kipigo cha bao 5-1, jana Jumapili katika Dimba la Mkapa.

"Yanga jana walicheza vizuri, walipambana kwa kiwango cha juu wakijua kwamba Simba ni timu kubwa, hilo ndilo liliwasaidia na sisi tukaingia kwenye mfumo wao tukapigwa tano.

"Vyumba waliacha wazi, kile chumba ambacho waliingia wachezaji wa Simba kipindi cha kwanza walibadilisha kipindi cha pili wakaingia chumba kingine, tuwaulize viongozi wa Simba nani aliwabadilishia chumba wachezaji?

"Hakuna kiongozi yeyote wa Simba aliyeko madarakani sasa hivi anayeweza kupambana na Eng. Hersi Said (Rais wa Yanga). Sio Try Again, siyo Mangungu sio Mo Dewji, hakuna hata mmoja wa kupambana na Hersi, uwezo wao ni mdogo na hawana mapenzi na timu. Hersi ana mapenzi na Yanga na anajua Yanga inahitaji nini na inataka kwenda wapi, tofauti nan a sisi.

"Yanga wana mfadhili, Simba wana mwekezaji, anayetakiwa kupata mafanikio zaidi ni nani? Mo Dewji atuachie timu yetu kwa sababu tangu amekuja hakuna mafanikio makubwa aliyoyafanya ambayo Simba hajawahi kuyafikia tangu awali.

"Simba alishawahi kumfunga Yanga bao 5, bao 6, ameshawahi kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, na Shirikisho Fainali lakini Mo hajavuka. Hatukuwa na pesa miaka hiyo lakini tulikuwa hatufungiwi bao nyingi na Yanga, wewe ni mdhamini unafungwa namna hiyo na Mfadhirili?

"Mo atuachie Simba yetu kwa sababu ametuletea viongozi anaowataka mwenyewe kwa maslahi yake. Mechi inayokuja Simba atafungwa bao 7 na Yanga, kuna mambo makubwa hatuwezi kuyasema ila Mo atuachie Simba yetu tutajipanga wenyewe.

"Leo wanatengeza sababu ya kumuondoa mwalimu, Robertinho hana kosa, viongozi ndio wameshindwa kupambana na Yanga nje ya uwanja, Hersi ana akili zaidi kuliko viongozi wa Simba. Mwalimu ndiyo amemlazimisha Manula kucheza? Simba haina viongozi wanaoweza kushindana na Yanga.

"Kipindi cha pili ndipo timu yetu imekufa, ikarudi kama tambala la kupigia deki, Mo aturudishie Simba yetu. Kama kweli wana mapenzi ya Simba, wajiuzulu, watuachie timu yetu. Hawawezi kupamba na Hersi atawafinyanga kila siku kama anavyotaka mwenyewe," amesema Mzee Masatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live