Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sh10 bilioni zahitajika timu za Taifa

Tanzania Taifa Stars UT Sh10 bilioni zahitajika timu za Taifa

Thu, 11 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya hamasa ya timu za Taifa Tanzania imesema kiasi kinachohitajika kwa ajili ya kuzichangia timu za taifa ni Sh10 bilioni.

Mwenyekiti wa kamati ya hamasa ya timu za Taifa, Theobald Sabi amesema kiasi kitakachokusanywa katika awamu ya kwanza ya michango hiyo kitakabidhiwa katika kipindi cha ndani ya miezi mitatu.

"Awamu ya kwanza itakamilika ndani ya miezi mitatu kwa hiyo kamati yetu itakabidhi michango ndani ya siku 90. Nitumie fursa hii kuwaomba wadau wachangie.

"Lengo hili la kukusanya kiasi cha Sh10 bilioni tutalifanikisha. Kamati hii ina majukumu matatu. La kwanza ni kukusanya fedha kutoka kwa wadau ambazo zitatumika kwa timu za taifa.

"Kuelimisha umma kuhusu uwepo wa timu za taifa na kuhamasisha umma kuhusu kuchangia timu za taifa. Kamati yetu imejiwekea mipango ya muda mfupi, wa kati na mrefu," alisema Sabi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live