Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sesko avuruga mipango Arsenal

Sesko Sesko avuruga mipango Arsenal

Thu, 13 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Arsenal imefuta mpango wa kusajili straika mpya kwenye dirisha hili baada ya kukataliwa na Benjamin Sesko.

Arsenal iliweka nguvu kwenye mchakato wa kunasa saini ya straika huyo wa Red Bull Leipzig. Na ilikuwa na uhakika wa kunasa saini yake kwa maana ya kulipa Pauni 55 milioni iliyoelekezwa kwenye mkataba wake kwa timu zinazomhitaji, zikilipa basi zinanasa huduma yake.

Hata hivyo, fowadi huyo amegoma na sasa amesaini mkataba mpya wa kubaki RB Leipzig. Si Arsenal pekee waliokutana na ugumu wa kumsajili fowadi huyo, bali wapinzani wao pia kwenye Ligi Kuu England, Manchester United na Chelsea nazo zimekwama kumnasa Sesko, ambaye mkataba wake mpya huko Leipzig umeripotiwa utafika tamati 2029.

Jambo hilo sasa limeifanya Arsenal kubadili mbinu zao kwenye usajili wa dirisha hili. Ripoti zinafichua kwamba kwa sasa, ishu ya kusajili straika mpya haipewi tena kipaumbele kwenye kikosi hicho cha kocha Mikel Arteta.

Kocha Arteta ameelekeza nguvu zake kwenye usajili wa mchezaji wa pembeni kuja kuongeza nguvu kwenye kikosi chake kabla ya msimu wa 2024/25 kuanza. Arsenal imekuwa ikifukuzia huduma za mawinga kadhaa, akiwamo mkali wa Sporting Lisbon, Marcus Edwards, wa Wolves, Pedro Neto na yule Nico Williams wa Athletic Bilbao.

Ukiachana na mawinga, Arsennal pia kwa sasa inataka kiungo, ambapo kwenye mipango yao yupo mkali wa Real Sociedad, Martin Zubimendi.

Kuna wachezaji kadhaa wataachana na Arsenal kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi. Aaron Ramsdale na Emile Smith Rowe ni miongoni mwa wachezaji ambao watafunguliwa mlango wa kutokea kwenye dirisha hili.

Eddie Nketiah na Leandro Trossard nao wanaweza kuondoka kama Arsenal itaweza kupata mtu mpya kwenye fowadi, lakini kitendo cha Sesko, kuwagomea kimefanya wabadilishe mawazo na kuhamia kwenye maboresho ya idara nyingine kikosini.

Chanzo: Mwanaspoti