Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sesko afunguka kuitosa Arsenal

Sesko Sesko afunguka kuitosa Arsenal

Sat, 15 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Straika, Benjamin Sesko amesema kusaini dili jipya RB Leipzig ni kitu cha maana zaidi kufanya kwenye maendeleo ya soka lake kuliko kwenda Arsenal.

Sesko aligomea nafasi ya kwenda kujiunga na miamba hiyo ya Emirates kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi kabla ya kumhuzunisha kocha Mikel Arteta kwa kuamua kusaini mkataba mpya wa kubaki kwenye kikosi cha RB Leipzig.

Arsenal ipo sokoni kusaka straika mpya na iliamini Sesko ni mtu mwafaka kwenda kujiunga na timu yake. Hata hivyo, staa huyo aligomea ofa hiyo.

Sesko, 21, alifunga mabao 18 katika msimu wake wa kwanza Bundesliga, alikiri kuanza kwa kasi ndogo kwa kuwa hakuwa amezoea mazingira ya Ujerumani kwa haraka, lakini baada ya muda alitulia na kuonyesha ubabe wake.

Alisema baada ya kusaini dili jipya: “Nimekuwa na mwaka wangu wa kwanza mzuri RB Leipzig na nina furaha kubaki hapa. Hii timu, klabu, mashabiki na jiji lenyewe, vyote vimekuwa na mvuto kwangu. Kusaini mkataba mwingine mapema kilikuwa kitu cha maana zaidi kwangu.

“Hata kama sikucheza au kufunga sana kwenye nusu ya kwanza ya msimu, lakini hii ni kitu muhimu kwenye maendeleo ya soka langu. Najiona nimeaminika zaidi kwenye klabu hiyo.”

Arsenal ilikuwa tayari kulipa Pauni 55 milioni ambayo ilibainishwa kuwekwa kwenye kipengele cha mkataba wa mchezaji huyo kama kutakuwa na timu itahitaji saini yake. Na sasa Arsenal imehamishia nguvu kwa straika wa Bologna, Joshua Zirkzee, ambaye bei yake ni Euro 40 milioni.

Chanzo: Mwanaspoti