Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Seseme ajishtukia Tabora United

Sesemeeeee Seseme ajishtukia Tabora United

Fri, 23 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kiungo wa zamani wa Kagera Sugar, Abdallah Seseme anayekipiga kwa sasa Tabora United, amejishtukia na kusema anapaswa kukaza buti kama mchezaji, lakini hata timu hiyo inapaswa kukomaa kwa vile anauona msimu huu kuwa ni mgumu zaidi kuanzia klabuni hapo katika Ligi Kuu Bara.

Nyota huyo alioyewahi kuwika Simba, amejiunga na Tabora akitokea Kagera ambako hakufunga bao zaidi ya kuasisti mabao manne, jambo linalompasua kichwa kuwa kwa sasa ana kazi ya ziada ya kufanya katika ligi iliyoanza wiki iliyopita na iliyoingia raundi ya pili wikiendi hii.

Seseme alisem amebaini kuna ushindani wa namba mkubwa ndani ya kikosi hicho katika eneo analocheza la kiungo kukiwa na Wanigeria, Morice Chukwu na Shedrack Asiegbu aliyemuona ni mzuri na anajituma, hivyo anampa changamoto ya kuwa bora zaidi.

"Japo tulifungwa mechi ya kwanza dhidi ya Simba kuna wachezaji wengi wazuri hawakucheza. Naamini huko mbele tutafanya makubwa. Ushindani wa namba unaanzia mazoezini kila mchezaji anatamani awe muhimu kwenye kikosi cha kwanza. Hilo linasaidia tutakapokutana na timu pinzani kufanya vizuri," alisema Seseme.

Vilevile ameizungumzia timu yake ya zamani ya Simba, akiamini kwamba ina wachezaji wazuri, lakini wanahitaji muda na pia kuuona ukubwa wa majukumu waliokabidhiwa.

"Simba ina mabadiliko makubwa, yanayohitaji uvumilivu kwa mashabiki, lakini wachezaji wana kazi ya ziada kuonyesha uwezo wa kuifaa timu yao," alisema.

Tabora ilianza msimu kwa kufungwa mabao 3-0 na Simba kwenye Uwanja wa KMC na kesho itashuka uwanjani tena ugenini kuumana na Namungo mkoani Lindi.

Chanzo: Mwanaspoti