Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yazitaka timu kuwachukulia wachezaji, makocha wa kigeni vibali

Uhamiaji House Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji

Tue, 24 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali kupitia idara ya Uhamiaji imezitaka timu za ligi kuu na zile za daraja la Kwanza nchimi, kuwachukulia vibali wachezaji na makocha wa kigeni wanaokuja kujiunga kwenye timu hizo.

Afisa habari wa Idara ya uhamiaji, Paul Msele, amevitaka vilabu kuhakikisha zinafuata sheria na taratibu za nchi na vibali hivyo ni kuanzia vile vya kufanya kazi na kuishi nchini.

"Tulishawaeleza chama cha mpira nchini TFF, maana ndio wadau wao wahakikishe wachezaji wa kigeni pamoja na makocha wanaowaletwa wanakumbusha hili suala, kwa hiyo vilabu ambao ndio waajiri wao lazima vihakikishe wanafanya kazi kwa utaratibu unaotakiwa kupitia idara ya kazi hali kadhalika kuishi hapa nchini" amesema

Kauli hiyo ya Idara ya Uhamiaji imekuja mda mchache tangu klabu ya Yanga iliposema imekamilisha ITC za wachezaji wake wote wa kigeni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live