Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaweka wazi mkataba wa Kocha Mpya Taifa Stars

Adel Amrouche 12.jpeg Serikali yaweka wazi mkataba wa Kocha Mpya Taifa Stars

Tue, 7 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Utamaduni, Sana na Michezo Mhe, Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuendeleza mchezo wa Soka nchini itamlipa mshahara mwalimu wa Timu ya Taifa (Taifa Stars), Adel Amrouche ambaye ni raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Algeria.

Hayo yamebainishwa wakati wa kumtambulisha Kocha huyo, Machi 07, 2023 Mtumba jijini Dodoma na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana aliyeambatana na Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Said Othman Yakubu .

Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Serikali inaamini Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limejiridhisha kuwa ni Kocha Bora atakayekuza soka la Tanzania.

"Ukitazama wasifu wa Kocha Adel utabaini uzoefu mkubwa alionao sio tuu katika kufundisha soka uwanjani, bali pia katika kuandaa Wataalamu wengine wa Soka, hivyo tumtumie vizuri ili asaidie timu yetu kufanya vizuri ndani na nje ya nchi"

Dkt. Chana ameongeza kuwa, Serikali inaendelea kuangalia uwezekano wa kupata Wataalamu katika michezo mingine ambapo ameeleza kuwa Wizara inaendelea kuimarisha Wataalamu wa michezo kupitia Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kilichoko wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.

Kwa upande wake Kocha Amrouche ameahidi kuwanoa wachezaji vyema ili kuiweka juu zaidi Tanzania katika ulimwengu wa Soka , huku akisisitiza ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali katika kufanikisha kazi yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live