Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yasisitiza umoja, uzalendo Simba na Yanga

Ndumbaroo Simba.heic Serikali yasisitiza umoja, uzalendo Simba na Yanga

Wed, 20 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro amewaomba Watanzania waziunge mkono timu za Simba na Yanga ambazo zinatarajiwa kucheza michezo ya Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika kwa kuwa ushindi wa timu hizo utaleta heshima kwa nchi, mpira wa Tanzania na timu zinazoshiriki.

Aidha, amewaonya baadhi ya Watanzania ambao wamekuwa na tabia ya kuzipokea na kuzishangilia timu ngeni zinapokuja kucheza na timu za Tanzania waache tabia hiyo kwa kuwa inarudisha nyuma juhudi kubwa za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye katika uongozi wa miaka mitatu amefanya mambo makubwa kuendeleza michezo nchini.

Dkt. Ndumbaro ameyasema hayo Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa mtandao mpya wa Simba SC uliopewa jina la "Simba Executive Network" ambao una lengo kukusanya fedha kwa ajili ya kuendeleza miundombinu ya Klabu hiyo.

"Natamani kuziona timu zote nusu fainali, inaleta heshima kwa nchi, inaleta heshima kwa mpira wetu na vilabu vyetu"-amesisitiza Dkt. Ndumbaro

Amesema Serikali haifurahishwi na tabia ya baadhi ya Watanzania ambao huwafanya wageni wajisikie nyumbani wanapokuja kucheza hapa nchini huku wakiibeza timu ya Tanzania jambo ambalo halina faida kwa maendeleo ya soka.

"Timu ambayo itajigeuza kuwa Kamati ya itifaki kwenda kupokea wageni Uwanja wa ndege tutashughulika nayo, wageni watapokewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) , ndivyo taratibu zinavyoelekeza na sio timu. Kuanzia mechi hizi kiongozi yeyote, Mwanachama au timu itakayofanya hivyo hatutaivumilia ", amesisitiza Dkt. Ndumbaro

Chanzo: www.tanzaniaweb.live