Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaruhusu nyota 10 wa kigeni kama kawaida

Serikali+pic Serikali yaruhusu nyota 10 wa kigeni kama kawaida

Tue, 11 Aug 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Oliver AlbertSERIKALI kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imebariki klabu za Ligi Kuu Bara kuendelea kusajili wachezaji 10 wa kigeni kutokana na wadau wengi kutaka iwe hivyo.

Hata hivyo Mwakyembe amezitaka klabu kufanya usajili wa wachezaji wenye viwango na si bora wachezaji.

"Klabu zetu hivi sasa ziko katika hekaheka za usajiliwa wachezaji wanaowataka kwa ajili ya msimu ujao.

"Nawatakia kila la kheri katika  usajili wao lakini mlete vifaa vya kuwafaa sio vifaa vya kuwavaa na kuwavuruga mkaishia kuvutana kwa malumbano yasiyo na tija kwenye mitandao na mikutano yenu badala ya kucheza soka" amesema Mwakyembe.

Mwakyembe amesema kutokana na mjadala waliouendesha wameona idadi ya wachezaji wa kigeni kwenye ligi hiyo ibaki 10 kama ilivyokuwa awali

"Kulikuwa na mjadala niliouanzisha kuhusu idadi ya wachezaji wa nje kwenye ligi zetu sio kwa soka tu ila na michezo mingine.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz