Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yampa maagizo Etoo juu ya Kocha mpya Cameroon

Etoo Samuel Etoo, Rais wa Shirikisho la Soka Cameroon

Thu, 2 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali nchini Cameron imemwamuru Rais wa Fecafoot Samuel Etoo kusaini haraka nyaraka za ajira ya kocha mpya wa timu ya Taifa ya Cameron Marc Brys.

Taarifa iliyotoka Jana inasema Serikali imempa Etoo hadi mwishoni mwa wiki hii awe ameshasaini nyaraka zote muhimu za kocha huyo na watumishi wengine wa benchi la Ufundi ili kocha huyo aanze harakati mapema ya kufuzu kombe la Dunia.

Ikumbukwe kocha Marc alitangazwa kuwa kocha wa Cameron na Serikali kuchukua nafasi ya Rigobert song,huku ikielezwa Etoo anapitia mazingira magumu kusimamia soka nchini humo kwani Serikali imekuwa ikiingilia baadhi ya maamuzi bila kumshirikisha samuel.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live