Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaipongeza TFF

Mkuu Pic Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Thu, 21 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Serikali ya Tanzania imelipongeza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa namna inavyoendelea kusimamia mchezo wa Soka.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa usiku wa leo Oktoba 21 kwenye utoaji wa Tuzo za wanasoka waliofanya vizuri kwa msimu wa Ligi Bara msimu wa 2020/2021 ambapo amealikwa kama mgeni rasmi.

Wakati akihutubia umma wa wadau mbalimbali waliojitokeza kwenye ukumbi wa JNICC, Dar es Salaam Majaliwa amesema;

“Tunawapongeza TFF, kwa kazi nzuri wanayofanya na tunataka waendelee kuboresha na kwenda sawa na namna mambo yanavyotakiwa kuwa,” amesema Majaliwa na kuongeza;

“Tumeweka utaratibu mzuri wa kuinua michezo na vipaji nchini ili tuweze kuwa na timu za taifa bora na zenye ushindani,” alisema.

Pia Majaliwa alizungumzia tuzo hizo zinazotolewa leo na kusema;

“Tuzo ni matokeo ya ubora ambao wahusika wameuonesha, hii inatoa hamasa kwq wachezaji na mimi nitashiriki kutoa tuzo hizi leo kama sehemu ya motisha kwa wale waliofanya vizuri zaidi,”  amesema Majaliwa.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz