Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaipongeza Simba suala la Katiba

Simba Katiba Ms Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo nchini (BMT), Nicolas Mihayo.

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baraza la Michezo Tanzania (BMT) limeipongeza Kamati ya Maboresho ya Katiba ya Simba kwa kufuata maelekezo yote yaliyotakiwa kufanywa kabla ya mabadiliko ya katiba.

Pongezi hizo zimetolewa na Nicholaus Mihayo aliyekuwa akimuwakilisha Katibu Mkuu wa BMT katika Mkutano Mkuu wa Wanachama unaoendelea katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere.

Mihayo ameongeza kuwa Serikali inapenda kuona maelekezo inayotoa yanafuatwa yote kwa wakati na ndicho tulichokifanya.

“Tunaipongeza Simba kwa kufuata maelekezo na kuyafanyia kazi maboresho ya katiba. Hili ni jambo la mfano kwa timu nyingine. Serikali inawatakia kila la kheri,” amesema Mihayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live