Serikali imeitaka timu ya taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ kujiandaa kikamilifu, kupata matokeo mazuri katika mchezo wa mwisho, wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON) dhidi ya Togo.
Twiga Stars itashuka dimbani keshokutwa kuivaa Togo katika mechi ya hatua ya pili itakayopigwa katika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es salaam.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Neema Msitha, amesema Twiga Stars inapaswa kufanya vizuri katika mechi hiyo muhimu na kukata tiketi ya kucheza fainali hizo.
Neema amesema Serikali, Watanzania kwa ujumla wapo bega kwa bega na timu kwa kutoa sapoti, hamasa na kuhakikisha matokeo mazuri, kushinda zo huo wa mwisho.
Timu inapaswa kupata matokeo mazuri yatakayoipa Tanzania nafasi ya kufuzu fainali,” amesema Neema.
Aisha Masaka anayecheza soka la kimataifa nchini Sweden amesema amekuja kuongeza nguvu kikosini na kuhakikisha Tanzania inashinda na kufuzu fainali.
Aisha amesema anawaomba mashabiki kuendelea kuisapoti timu, kuiombea na kutoa hamasa itakayowapa nguvu ya kupeperusha vizuri bendera ya nchi.
Twiga Stars ilifuzu hatua ya pili kuwania kufuzu WAFCON kufuatia ushindi wa Penalti 4-2 dhidi ya lvory Coast baada ya kutoka sare ya mabao 2-2, katika mchezo wa kwanza Stars ilipoteza kwa mabao 2-0 kabla ya ushindi wa mabao 2-0.
Iwapo Twiga Stars itashinda dhidi ya Togo, itakata tiketi ya kucheza fainali za WAFCON zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.