Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yaihakikishia Simba usalama Afrika Kusini

Simba Orl Serikali yaihakikishia Simba usalama Afrika Kusini

Thu, 21 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa amewatoa hofu mashabiki wa soka wanaotaka kwenda Afrika Kusini kuishangilia Simba SC katika mchezo wa raundi ya pili robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kuwa watakuwa salama.

“Niseme tu kwamba sisi kama Serikali tunafuatilia kwa karibu usalama wa timu na hivi ninavyoongea nimemteua msaidizi wangu Mkurugenzi wa Michezo ili aweze kuniwakilisha kusimamia hili” amefafanua Mchengerwa.

Aidha, amesema Watanzania na raia wa Aafrika Kusini ni ndugu wa muda mrefu hivyo ni mategemeo kuwa hakutakuwa na jambo lolote linaloweza kuhatarisha usalama.

Ameeleza kuwa katika mechi hiyo Timu ya Simba inakwenda kushindana siyo kushiriki ili kuliwakilisha taifa ambapo amewataka wachezaji kucheza kwa weledi na ari kubwa ili ipige hatua katika hatua inayofuata hatimaye irudishe kombe nyumbani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live