Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yagoma kuipa Simba ndege kwenda Misri

Simba Zenzjis Serikali yagoma kuipa Simba ndege kwenda Misri

Wed, 3 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma 'Mwana FA amesema, mara baada ya serikali kusafirisha mashabiki 48 wa Yanga kwenda Afrika Kusini, Klabu ya Simba imetuma maombi kuomba ndege ili iwasafirishe mashabiki wake kwenda kuishangilia timu yao nchini Misri.

Mwana FA amesema kuwa Serikali inashughulikia maombi hayo ya Klabu ya Simba ambayo yatawawezesha mashabiki wa klabu hiyo kupata nafasi ya kwenda kuishabikia klabu yao nchini Misri na watapewa majibu na utaratibu.

Mwana FA ameyasema hayo jana nje ya ukumbi wa Bunge ambapo amesema kuwa wameshafanya hivyo kwa klabu ya Yanga ambapo wamefanikisha mashabiki 48 wa klabu hiyo ya Yanga siku ya jana April 1, 2024 kwenda pretoria Nchini Afrika ya Kusini kushuhudia mechi ya marudiano kati ya Klabu hiyo ya Yanga na Klabu ya Mamelodi Sundowns ya nchini humo.

"Tumewaaga wapenzi 48 wa Yanga ambao wamesafiri kwa njia ya barabara kwenda Afrika Kusini kushuhudia mchezo wa marudiano wa Mamelodi Sundowns dhidi ya Yanga.

"Baada ya jambo hilo, klabu ya Simba nayo imeleta maombi yake ambayo tunayashughulikia na ninaamini wapenzi wa Simba pia watapata fursa ya kwenda kushuhudia mechi ya marudiano ya Al Ahly dhidi ya Simba.

"Ni jambo la kiutaratibu, klabu inatakiwa iseme inataka nini halafu serikali tutaona kama lipo ndani ya uwezo wetu kwa wakati huo na tunayafanya. Kama ambavyo tulifanya kwa klabu ya Yanga, maombi ya klabu ya Simba tumeyapokea na tunayafanyia kazi," amesema Mwana FA.

Akifafanua kuhusu maombi hayo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Gerson Msigwa amesema kuwa Serikali haijaitenga Simba wala timu nyingine yoyote badala yake iko nayo bega kwa bega kuisapoti.

"Serikali haijaitenga Simba, tunepokea maombi maombi yao na tutawapa utaratibu. Kwa sasa Serikali haina uwezo wa kuwapa Simba ndege kama walivyoomba, lakini niwahakikishie kwenye bajeti yao walioiwasilisha kwetu kuomba sapoti ya mashabiki kusafirishwa na Serikali tutawapa kiasi kilekile sawa na ambacho tumewapa Yanga kwenda Afrik Kusini.

"Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuipa nguvu michezo na hususani timu zetu zinazoshiriki michuano mikubwa, tutaendelea kufanya hivyo," amesema Msigwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live