Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali ya Tanzania yapiga marufuku kuvaa jezi za Mamelodi na Al Ahly

Mamelodi Na Al Ahly Mamelodi Sundowns na Al Ahly.

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro amepiga marufuku mashabiki wa soka wa nchini Tanzania kuvaa jezi za timu pinzani (Mamelodi Sundowns ama Al Ahly) kwenye michezo dhidi ya CAFCL ambazo zimepangwa kucheza na Simba na Yanga za Tanzania.

Ikumbukwe kuwa, kwenye hatua ya robo fainali ya CAFCL, Simba imepangwa kucheza na Al Ahly ya Misri wakati Yanga ikipangwa kucheza na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa Zainabu Rajabu ameripoti kuwa Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Dr. Dmas Ndumbaro amesema kuwa, Serikali itasimamia suala la uzalendo kwa yoyote atakayekiuka.

“Sisi kama Serikali tumeweka mkakati wa kuchunguza shabiki yoyote ambaye atakaye kwenda kinyume na uzalendo kuelekea mechi za CAFCL za Yanga na Simba"

"Tukikuona uvaa jezi ya Mamelodi au Al Ahly tutakuchukulia hatua vile inastahiki," amesema Dkt. Damas Ndumbaro.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live