Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali itimize wajibu wake kabla ya kuomba sapoti ya shabiki

Majaliwa Stars Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipotembelea mazoezi ya Stars

Wed, 10 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wadau mbali mbali wa Soka nchini wameitaka Serikali ibebe jukumu la kuihudumia Timu ya Taifa na sio kuwaachia mzigo Shirikisho la Soka TFF kuwa ndio mtoaji wa huduma zote za timu hiyo.

Yamezungumzwa hayo baada ya hivi karibuni Serikali kufanya kila jitihada kusimama na Stars ili tu kuhakikisha inafanya vyema katika michezo yake miwili ya hatua ya Makundi iliyobaki kutafuta nafasi ya kwenda hatua inayofuata ili wawezer kufuzu kwa Fainali za kombe la Dunia Qatar 2022.

"Tumeona fedha nyingi zimechangwa, hamasa imetolewa lakini hili halitoshi timu ya Taifa ni kitu kingine, hapa inatakiwa hili linalofanyika liwe linafanyika wakati wote hatutakuwa na haja ya kutafuta hamasa lakini wao wanakwepa mzigo wanasubiri nyakati kama hizi za mwisho ndipo wanajitokeza"

"Shabiki anakuja tu kuongeza thamani kwa kile ambacho umeshakitengeneza kwa muda mrefu hivyo tusiwabebeshe wachezaji lawama kupitia mgongo wa sapoti ya shabiki"

Taifa Stars inashuka dimbani Novemba 11, kuvaana na DR Congo katika mchezo wa kundi J.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live