Serie A imejihakikishia kuwa na vilabu vitano katika Ligi ya Mabingwa msimu ujao baada ya timu zake kupata nafasi mbili za juu katika msimamo wa mgawo wa UEFA huku vilabu vikiongezwa kutoka 32 hadi 36 kwa msimu ujao.
Roma na Atalanta zote zimetinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Europa siku ya Alhamisi huku Fiorentina ikiwa katika nafasi nne za juu za Ligi ya Europa Conference.
Hiyo ina maana kwamba Italia imekusanya jumla ya pointi 19.428, mbele ya Ujerumani wenye pointi 17.928 na Uingereza wenye pointi 17.375 na itachukua moja ya nafasi mbili za ziada kwenye mashindano.
Ligi ya Mabingwa itakuwa na timu 36 katika hatua ya makundi kuanzia msimu ujao, nne zaidi ya ya msimu huu.