Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sergio Busquets atangaza kustaafu Timu ya Taifa

Sergio Busquets Sergio Busquets atundika daluga Hispania

Fri, 16 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Barcelona na Timu ya Taifa ya Hispania, Sergio Busquets ametangaza kustaafu kucheza soka la Kimataifa.

Sergio Busquets amecheza mechi 143 za timu ya taifa ya Hispania huku akitwaa mataji mawili makubwa akiwa na uzi wa Hispania ikiwemo Kombe la Dunia (2010) na Mataifaya ya Ulaya (EURO 2012).

Busquets anastaafu Timu ya Taifa akiwa ni miongoni mwa wachezaji watatu waliocheza mechi nyingi nyuma ya Sergio Ramos aliecheza michezo (180) na Iker Casillas (167).

Wakati huo huo Busquets anafikiria kuhusu mustakabali wake ndani ya FC Barcelona lakini Barcelona wanategemea kiungo huyo kumalizia msimu huu.

Barca wanataka Busquets abaki Camp Nou kwa mwaka mmoja zaidi baada ya msimu huu lakini kuna ofa kutoka Inter Miami inayoshiriki Ligi ya Marekani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live