Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sergio Aguero sasa anafikiria kustaafu?

Sergio Aguero Sergio Kun Aguero

Sat, 13 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nyota wa Barcelona, Sergio Aguero ameripotiwa kuwa sasa anapanga kustaafu soka la kulipwa baada ya kugunduliwa kuwa ana tatizo la moyo.

Nyota huyu alilazimika kupelekwa hospitali wakati wa mechi dhidi ya Alaves mwezi uliopita.

Suala hili liliibua hisia tofauti tofauti juu ya hali ya Sergio Aguero, huku ripoti kadhaa zikiripoti kuwa amepatikana na tatizo la moyo na hivyo yupo kwenye mipango ya kustaafu.

Hata hivyo, nyota huyu amejitokeza hadharani na kukanusha uvumi juu ya mpango wake wa kutaka kustaafu.

“Kwa sababu ya uvumi, ninafuata maelekezo ya madaktari wa klabu. Ninafanya vipimo na matibabu, na ninaona maendeleo ndani ya siku 90.” – Sergio Aguero akinukuliwa na na BBC

Nyota huyu alikuwa ni mfungaji bora wa wakati wote alipokuwa na Man City kabla ya kuungana na Barcelona kama mchezaji huru mwezi Julai.

Nyota huyu amefunga goli moja pekee katika mechi tano alizocheza Barcelona tangu kuwasili kwake, akiukosa mwanzo wa msimu huu kwa sababu ya shida ya majeraha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live