Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sergio Aguero majanga tena Barca

AGUERO ONE Sergio Aguero akitolewa uwanjani baada ya kupewa huduma ya kwanza

Tue, 2 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa ni wiki chache tu tangu arejee kutoka katika majeraha, mshambuliaji wa Barcelona, Sergio Kun Aguero anatazamiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu baada ya kukutwa na tatizo katika mishipa yake ya moyo jambo linalopelekea  wakati mwingine apumue kwa tabu.

Taraifa ya Aguero kutakiwa kuwa nje ya uwanja imekuja baada ya daktari anayemtibia kwa sasa Dkt. Josep Brugada kuthibitisha kuwa nyota huyo anapaswa kuendelea kupata matibabu chini ya uangalizi maalum.

Aguero alipata tabu ya kupumua alipokuwa uwanjani wakati Barcelona ilipokuwa inacheza na Derpotivo Alaves kwenye La Liga Jumamosi ya Oktoba 30, 2021 jambo lililomfanya ashindwe kuendelea na mchezo na kutolewa dakika 41.

Aguero amejiunga na Barca msimu huu akitokea Manchester City kwa uhamisho huru, na tangu ajiunge na miamba hiyo ya Hispania amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live