Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serengeti Boys yatinga nusu fainali CECAFA U17

Serengeti U17 Kikosi cha Serengeti Boys

Tue, 11 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya taifa ya Tanzania imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya michuano ya CECAFA U17 baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Somalia jana Uwanja wa Abebe Bikila Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Mabao ya Serengeti Boys katika mchezo huo wa mwisho wa Kundi A yote yamefungwa na Sylvester Otto dakika ya 75 na 80 na kwa matokeo hayo wanamaliza na pointi sita kufuatia awali kuwafunga wenyeji, Ethiopia 3-2.

Sasa Serengeti Boys itamenyana na Sudan Kusini katika Nusu Fainali Jumatano, wakati Uganda ambao ndio mabingwa watetezi watacheza na Somalia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live