Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Senzo awataja Manula, Chama

Manula Pic Data.png Senzo awataja Manula, Chama

Mon, 24 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

MSHAURI Mkuu wa masuala ya uongozi wa Klabu ya Yanga, Senzo Mbatha amesifia viwango vya wachezaji wa Simba, Aishi Manula na Clatous Chama walivyovionyesha kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika.

Senzo aliandika kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwapongeza wachezaji hao baada ya kupambana kuhakikisha wanaisaidia timu yao iliyoishia hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.

“Nawaheshimu wachezaji wote niliofanya nao kazi, ukiwaangalia kupitia mechi za CAF, Manula, Kapombe (Shomary), Chama, Luis (Miquissone), Edward Manyama wa Namungo na Wawa (Paschal) wamefanya vizuri na wanahitaji hatua kubwa zaidi.”

Kauli yake iliungwa mkono na baadhi ya wachangiaji katika ukurasa wake baada ya kuonyesha kukubali kile kilichofanywa na wachezaji wa timu pinzani.

Senzo kabla ya kujiunga Yanga alikuwa Mtendaji Mkuu wa Simba na alifanya kazi na wachezaji hao huku akiwa sehemu ya mafanikio katika klabu hiyo kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara pamoja na kufika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akiwa Yanga kwa sasa amekuwa mshauri wa uongozi wa klabu hiyo inayopambana kujiimarisha kuwania kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao.

Related Mikakati Simba kuiua Dodoma Jiji kuanza leo PRINCE DUBE: Huyu jamaa ni zaidi ya moto UCHAMBUZI: Tushirikiane kukomesha uhuni huu katika ligi zetu! Yanga wapata mchongo mpya

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz