Sat, 30 Jul 2022
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Yanga, Senzo Mbatha amefikia makubaliano na klabu hiyo ya kutoongeza mkataba wake baada ya miaka mitatu ya utumishi wake.
Kwa mujibu wa taarifa, mkataba wa Senzo utafikia mwisho Julai 31, 2022.
Katika taarifa ya Klabu ya Yanga imesema kuwa Senzo ametoa taarifa kwa Uongozi wa Yanga kuwa kuondoka kwake ni kutokana na sababu za kifamilia.
Klabu ya Yanga imemteua Wakili Simon Patrick kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa mpito (Interim Chief Executive Officer).
Chanzo: www.tanzaniaweb.live