Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Senzo CEO mpya Yanga

Senzoooooooo Kaimu Mtendaji Mkuu wa Yanga, Senzo Mazingisa

Tue, 31 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela leo Agosti 31, 2021 amemtangaza, Senzo Mbatha kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu (C.E.O) wa Klabu hiyo atakayesimamia mchakato wa mabadiliko kufikia mwisho na aliyekuwa Kaimu Katibu Mkuu wa Klabu hiyo, Hajji Mfikirwa atakuwa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala.

Fredrick Mwakalebela ametangaza hayo baada ya Katiba ya Yanga kubadilishwa kutokana na wanachama wa Klabu hiyo kupitisha mchakato wa mabadiliko kwa asilimia mia.

Miaka kadhaa iliyopita Wazee wa Yanga walimkataa Mkenya Nagi aliyeletwa na Yusuf Manji ili awe CEO wa klabu hiyo wakidai nafasi kubwa kama hiyo haiwezi kushikwa na raia wa kigeni.

Senzo alikuja kwa mara ya kwanza nchini kufanya kazi na Simba SC, wapinzani wakuu wa Yanga, lakini akahama na kuhamia Yanga kama Mshauri mkuu na hivi sasa amekamata wadhifa wa juu kabisa ndani ya klabu hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live