Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Senegal wabeba Ubingwa wa AFCON U20

Senegal U20.jpeg Kikosi cha Senegal U20 wakifurahia ubingwa

Sun, 12 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya taifa ya Senegal, 'Simba Wadogo wa Teranga' wamefanikiwa kutwaa Kombe la Mataifa ya Vijana kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya Gambia jana Uwanja wa Kimataifa wa Cairo Jijini Cairo nchini Misri.

'Simba hao Wadogo wa Teranga' jana wamecheza Fainali ya nne ya AFCON U20 baada ya kushika nafasi ya pili katika Fainali za 2015, 2017 and 2019.

Na hili ni taji la pili kwa la Afrika ndani ya miezi miwili baada ya mapema Februari kutwaa Kombe la Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) kwa ushindi wa penalti 5-4 kufuatia sare ya 0-0 na wenyeji, Algeria Uwanja wa Nelson Mandela Jijini Algiers.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live