Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Selemani Mwalimu fundi atafunga sana

Seleman Mwalimu Gomez Asajiliwa Fountain Gate Selemani Mwalimu fundi atafunga sana

Thu, 12 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Selemani Mwalimu (25) top Scorer wa Zanzibar Msimu uliopita 2023-24 hii mechi ya tatu namtazama akiwa ndani ya Jezi ya Fountain Gate FC, mechi tatu kafunga magoli mawili mpaka sasa kwenye Ligi Kuu kuanzia mechi ya Simba kisha Namungo pamoja na leo dhidi ya Ken Gold! Kama akiendelea hivi atafunga na kutengeneza nafasi nyingi sana ijapokuwa yupo kwenye Timu ya Daraja la kati.

Mwalimu faida kubwa ambayo ataipata Msimu huu ndani ya Fountain Gate ni uwepo wa Dickson Ambundo, Salum Kiimbwa, Ediger William na Abal Kassim ambao wana uwezo mkubwa pia wa kutengeneza nafasi eneo la mwisho na mechi hizi tatu walizocheza hadi sasa hilo limeonekana, kama msimu jana alikuwa Mfungaji Bora wa Zanzibar akiwa na Magoli 20 basi mwaka huu ndani ya NBC PL anaweza kuweka hata Nusu ya Magoli hayo

Fountain Gate wana mchanganyiko wa wachezaji bora vijana ambao kwa msimu huu watakuwa sehemu nzuri sana iwapo wataendelea kuimarika na kujenga Timu yao huku wanapata ushindi taratibu, Kocha wao Mkuu kwa sasa Mohamed Muya anahitaji utulivu tu ili kuendelea kupata matokeo mazuri! Fountain Gate mpaka sasa wamecheza mechi tatu na wameshinda mbili kati ya hizo.

Simply! Selemani Mwalimu ukitazama utulivu wake eneo la mwisho, uharaka na usahihi wa maamuzi kwenye nafasi ambazo anapata ndani ya uwanja unaona kabisa kuna magoli mengi sana kama atapata mipira mingi kutoka kwa wachezaji wa nyuma yake, nasubiri kumuona zaidi kwenye mechi nyingine zijazo za Ligi Kuu na mashindano mengine! Talent nyingine ya kutazama ndani ya NBC PREMIER LEAGUE Msimu huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live