Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sebastien Haller: Ten Hag ni Kocha bora, United wanawaza matokeo tu

Sebastien Haller Mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Sebastien Haller

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Sebastien Haller amemtaja kocha wa Manchester United kuwa ni miongoni mwa makocha bora sana.

Anaamini pale Manchester United anapambana sana kuibadili timu yake lakini kwasababu mashabiki wanataka matokeo ya haraka wakati mwingine wanamtoa kwenye mipango yake.

"Ten Hag anawekeza muda wake na nguvu zake ili kupata kitu kizuri kitoka kwenye timu yake, hii ni England na Manchester United, watu hawataki kujua nini kinaendelea nyuma ya pazia, wanachotaka ni matokeo tu" - Haller

"Nilipokuwa Utrecht, alikuwa jirani yangu, huyu mtu haachi kufanya kazi, hiki ndio kitu pekee anachokifanya, na anataka kufanya vizuri".

"Unahitajika kuzoea mazingira na nina uhakika atafanya mambo mazuri na tayari anayo, namtakia kila lakheri, namshukuru sana."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live