Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sean Dyche ndio mkombozi wa Everton?

Sean Dyche Win Vs Gunners.jpeg Kocha mpya Everton, Sean Dyche

Sun, 5 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Everton baada ya kukaa kwa takribani siku 105 bila kupata ushindi kwenye ligi kuu ya Uingereza hatimae imefanikiwa kupata ushindi wa mbele ya vinara wa ligi kuu ya Uingereza klabu ya soka ya Arsenal ikiwa chini ya kocha mpya Sean Dyche alietambulishwa wiki hii kuchukua nafasi ya Frank Lampard.

Klabu ya Everton imefanikiwa kuifunga klabu ya Arsenal nao 1-0 katika mchezo uliopigwa katika dimba la Goodson Park mapema siku ya Jumamosi Huku vijana wa Sean Dyche wakiwa kwenye ubora mkubwa kukabiliana na klabu ya Arsenal.

Vijana wa Sean Dyche ambaye ameisimamia klabu hiyo katika mchezo wa kwanza walikua kwenye ubora mkubwa kwani waliweza kuwazuia klabu ya Arsenal isiweze kupata bao katika mchezo huo, Jambo ambalo limekua gumu kwa vigogo mbalimbali katika ligi kutokana na ubora waliokua nao.

Everon waliweza kupata bao pekee katika mchezo huo kupitia kwa beki wake James Tarkowski ndani ya dakika ya 60 ya mchezo na kuweza kufanikiwa kuzuia bao hilo mpaka mwisho wa mchezo huo, Hii inakua mara ya kwanza kwa Everton kushinda mchezo wa ligi kuu ya Uingereza tangu tarehe 22 Oktoba waliposhinda dhidi ya klabu ya Crystal Palace.

Klabu ya Everton sasa imefanikiwa kutoka kwenye nafasi ya 19 kwenye hatari ya kushuka daraja na kupanda mpaka nafasi ya 17 wakiwa na alama 18 katika michezo 21 waliyocheza mpaka sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live