Kocha wa kimataifa wa Uingereza na mchezaji wa zamani wa vilabu vya Chelsea,Fulham, na Tottenham Scott Parker amefukuzwa kazi tena akiwa kama kocha wa klabu ya Club Brugge.
Kocha Scott Parker amekutana na kadhia hiyo baada ya klabu yake ya Club Brugge kutupwa nje ya michuano ya ligi ya mabingwa ulaya na klabu ya Benfica, Huku klabu hiyo ikiwa ilifanya vizuri kwenye hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa ulaya ikimaliza kama kiongozi wa kundi.
Klabu ya Club Brugge chini ya Scott Parker imetupwa nje ya michuano ya ligi ya mabingwa ulaya kwa kipigo cha aibu kwani jana walifungwa mabao matano kwa bila katika dimba la Estadio da Luz, Hiyo ni baada ya kufungwa kwao mabao 2-0 mchezo wa kwanza hivo kutolewa kwa jumla ya mabao 7-1.
Kocha huyo pia amekua na wastani mbovu wa kupata matokeo tangu atue klabuni hapo ambapo amedumu kwa jumla ya miezi mitatu tu, Kwani kwenye michezo 12 aliyoiongoza klabu hiyo ameshinda michezo miwili tu, sare 6, na vipigo vinne jambo ambalo halijawafurahisha waahiri wake.