Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Scott MCTominay afunguka jambo Man Utd

Scott Mctominay N0mkj6j067zc121admgcdk3kj Scott MCTominay afunguka jambo Man Utd

Wed, 13 Dec 2023 Chanzo: Dar24

Kiungo kutoka nchini Scotland Scott MCTominay amesema wachezaji wa Manchester United wako nyuma ya Kocha, Erik ten Hag, licha ya klabu hiyo kutokuwa na matokeo ya kuridhisha katika mechi za hivi karibuni.

McTominay amesema kuwa hali katika chumba cha kubadilishia nguo imekuwa “sawa” hakuna chochote kibaya kwa Ten Hag.

Ni jukumu la wachezaji,” alisema MCTominay akinukuliwa na Sky Sport.

“Wachezaji wanajua hilo pia. Tumekuwa na wachezaji wengi wa ajabu na hivi sasa tuko kwenye hatua ambayo tuna wahusika wakubwa kwenye chumba cha kubadilishia nguo.

“Si tu kama baadhi ya makocha wengine ambapo imekuwa sumu kidogo wakati mwingine, wachezaji wapo nyuma ya kocha.

“Nimesema katika mahojiano mengine mengi na ndivyo itakavyokaa. Tumepata timu ya ajabu ya makocha pia inaweza kupotea kwa tafsiri ya kile wachezaji wanachofikiria na kinachosemwa nyuma ya milango, tunataka tu kufanya vyema kwa klabu ya soka.”

Kichapo cha Jumamosi (Desemba 09) dhidi ya Bournemouth kilikuwa cha 11 kwa United katika mechi 23 pekee msimu huu

Chanzo: Dar24