Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Scanda: Kama Kocha Stars atachwa kupangiwa kikosi, Fei Toto lazima aitwe

Feisal Leo Kiungo wa Aam FC, Feisal Salum "Fei Toto"

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama kocha wa Timu ya Taifa ataita wachezaji yeye mwenyewe kwa kuwaona basi jina la Fei Toto haliwezi kukosa. Kama tutaacha Nongwa na Chuki basi huyu ndiye mido bora kwenye ligi yetu, tunapambana kwa chuki kumshusha lakini mvua haizuiliki.

Watu wa Yanga wanatamani Fei asinyanyue hata mguu, Juzi kaifundisha Mido yote namna mido inacheza, kutoka kwenye Ufei Toto hadi TICHA FEI. Fundisha sana kazi hawa kina Aucho, fundisha sana kazi kina Mudathir ni vile hawaji hadharani kusema ila wanajua jinsi gani inauma.

Yule ambaye hukata jina lake timu ya Taifa kwa kushirikiana na Wahafidhina wa Jangwani Roho zinawauma mnoo. Yaani wanatamani wakampige mganga sababu hawafanikiwi kumshusha huyu Mwamba. Yaani kwa kifupi ni matusi ya hadharani, huu ni mchezo wa Nje.

Ile Kamati iloacha kumfungia Aucho na Kumfungia Kamwe eti haijaona Makosa ya Aucho juzi walikua wanajificha Chooni, Aibu baba, aibu wanangu, soka letu limejaa masela wanaofanya kazi kwa Upepo. Aucho hakustahili kucheza hii mechi, ni dhulma tu ndio imemfanya atokee Kwenye kikosi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live