Aliyekuwa kiungo wa klabu ya Simba Ismael Sawadogo amesema anaidai klabu ya Simba mshahara wa miezi mitatu na nusu sasa na mara zote viongozi wamekua wakimpiga chenga na kumpa ahadi za uongo.
Akizungumza Sawadogo amesema;
“Bado nina mkataba wa miezi sita na Simba ambao tulikubaliana kulipana mshahara kila mwezi hadi nitakapomaliza, lakini imekuwa tofauti kwani wanakwenda kinyume na makubaliano,”
“Nawadai mshahara wa Juni hawajaniingizia na tayari nimeongea na Mwanasheria wa Simba, Hossea lakini jibu lake ni kwamba nitatumiwa kesho maongezi yalifanyika kabla hawajasafiri kwenda kwenye maandalizi ya msimu mpya.” Sawadogo alisema pia amewatafuta viongozi wa juu ikiwemo kuwatumia ujumbe lakini hawajibu.
Sawadogo alisajiliwa na Simba wakati wa Dirisha dogo la msimu uliopita lakini akashindwa kuendana na kasi ya Simba na kudumu kwa miezi Sita tu kabla ya kuoneshwa mlango wa kutokea.