Yani Zabona Mwayombya amefutiwa kadi,aliyoonyeshwa na Mwamuzi Ahmed Arajiga baada ya kuonekana ni kweli mchezaji huyo wa Tanzania Prisons aliangushwa na nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto!
Ahmed Arajiga alimuonyesha Zabona kadi ya pili ya njano na kuwa nyekundu kwa madai ya kuonekana alijiangusha!
Swali langu ni je, kwa kuwa kitendo cha Mwayombya kutolewa kwa kadi nyekundu kuliipunguzia faida waliyokua nayo Prisons ya kuwa 11 dhidi ya 10 ya wachezaji wa Yanga!
Je Mwamuzi ambaye aliidhoofisha Prisons yeye ameathirika vipi kutokana na yeye kukosa umakini katika maamuzi yake?
Iwapo Arajiga angekuwa makini, tafsiri yake kama si penati basi Prisons wangepata faida ya faulo ambayo pengine wangetumia pigo hilo kujipatia bao la kusawazisha!tafsiri yake Mwamuzi amechangia pengine Maafande kushinda kuokota alama moja ambayo ingekuwa na maana kubwa kwao!
Timu nyingi zinagharamika kutokana na maamuzi ya hovyo ya Waamuzi ambao pamoja na hayo wao maisha yao yanaendelea kama kawaida!