Timu ya Afrika Kusini iliyomaliza katika nafasi ya tatu ya Fainali za 34 za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ imepokewa kishujaa na wadau wa soka nchini humo.
Kwa mujibu wa vyombo mbalimbali vya habari vya Afrika Kusini, katika Kiwanja cha Kimataifa ha Ndege cha Tambo Mbeki, timu hiyo ilipokewa na Waziri wa Michezo, Zizi Kodwa.
Taarifa hizo zimeongeza kuwa kila mchezaji wa timu hiyo atapata Dola za Marekani 52,000 (sawa na Sh milioni 131) baada ya kushika nafasi ya tatu katika Fainali hizo nchini Ivory Coast.
Waziri Kodwa amewapongeza wachezaji hao na kusema kuwa wameitoa kimasomaso nchi yao.
“Kwa mara nyingine tena nataka kumshukuru kocha kwa kutuwezesha kufika hapa. Kwa kweli Bafana Bafana kwa muda mrefu haijawahi kufika hatua hii,” amesema.
Rais wa Shirikisho la Soka Afrika Kusini (SAFA), Dk Danny Jordaan amemshukuru kocha wa timu hiyo, Broos, Rais wa CAF, Dk Patrice Motsepe na watu wa Ivory Coast kwa kufarikisha kwa kiasi kikubwa Fainali za ‘AFCON