Mataifa mawili ya Afrika yamefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia la wanawake inayoendelea nchini Australia na kupeperusha vyemba bendera ya Afrika.
Afrika Kuisni ilitinga hatua hiyo baada ya kuifunga Italia mabao 3-2 lakini kwa upande wa Nigeria licha ya kutoka suluhu dhidi ya Ireland ilifanikiwa kuvuka.
Ushindi kwa Afrika Kusini uliwahakikishia alama 4 na kuifanya timu hiyo kushika nafasi ya pili kwenye kundi G nyuma ya Sweden akiwa na alama 9, bila ya kupoteza mchezo hata mmoja huku Nigeria ikimaliza kwenye kundi B ikiwa na alama 5 akishinda mchezo mmoja dhidi ya Australia na kutoa sare michezo miwili.
Thembi Kgatlana, ameibuka shujaa wa Afrika Kusini kwenye mchezo wa leo baada ya kuwafunga midomo wapinzani wao dakika za mwishoni huku akipeleka kilio kwa mahasimu wao ambao walikuwa juu kwa alama mbili kabla ya mchezo huo kuchezwa, licha ya kuutawala mchezo kwa asilimia 62 kwa 38 lakini bado walikubali kichapo kutoka kwa watoto wa Mandela.
Baada ya timu hizo kuingia 16 bora Afrika Kusini itacheza dhidi ya Uholanzi huku Nigeria ikicheza dhidi ya England Agosti 7.
Timu za Afrika zimethibitisha uwezo wake katika michuano mbalimbali jambo ambalo linaiheshimisha bara letu kwenye anga za kimataifa baada ya Morocco kukiwasha kwenye fainali zilizofanyika Qatar.