Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saudia yatibua mashabiki Kombe la Dunia

Kombeeee Saudia yatibua mashabiki Kombe la Dunia

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mashabiki wa soka wamechukizwa baada ya Saudi Arabia kuthibitisha maombi yao ya kuwa wenyeji wa fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwaka 2034.

FIFA ilitangaza kuwa wenyeji wa fainali za Kombe la Dunia zitazofanyika mwaka 2030 zitakuwa Uruguay Argentina, Paraguay, Uhispania, Ureno na Morocco ndio.

Sasa Saudi Arabia tayari imefichua mipango ya kuandaa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2034 katika muda wa miaka 11 - baada ya kushindwa katika kinyang'anyiro cha kuwania uenyeji wa fainali za mwaka 2030.

Chama cha soka cha Saudi (FA) ilitoa taarifa rasmi; "Leo, tunaingia katika sura mpya inayofuata ya soka la Saudi, tunakusudia kutoa zabuni ya kuandaa Kombe la Dunia la FIFA nwaka 2034. Zabuni yetu imechochewa na safari ya mabadiliko ya Saudi Arabia, shauku ya mashabiki wetu, na kujitolea kwa ajili ya mashindano haya makubwa duniani."

Nalo Shirika la Habari la Saudia imemuomba mfalme wa taifa hilo kuiridhia maombi yao: "Mtukufu mfalme, Tunashauku ya kuandaa fainali za Kombe la Dunia mwaka 2034 ni taswira ya mwamko wa kina uliofanyiwa kazi katika ngazi zote, ambao umeifanya kuwa kituo cha uongozi cha kimataifa cha kuandaa michuano hiyo. matukio makubwa na muhimu zaidi ya kimataifa katika nyanja mbalimbali, pamoja na uwezo ulio nao. Pia kutokana na kuwa na vipengele vya kiuchumi na urithi mkubwa wa kitamaduni."

Lakini mashabiki wa soka Duniani hawajafurahishwa na uwezekano wa Saudi Arabia kuandaa fainali za Kombe la Dunia kutokana na hali ya hewa kwani itafanya mashindano hayo kufanyika katika majira ya joto jambo ambalo halitawezekani.

Ikumbukwe Qatar ilipotuma maombi ya uenyeji wa fainali za Kombe la Dunia yaliyofanyika mwaka jana huku kukiwa na mvutano mkubwa kutokana na hali ya hewa la taifa hilo.

Lakini baada ya Qatar kukubaliwa na FIFA kuandaa fainali hizo walibadilisha kutoka majira ya joto hadi msimu wa baridi kwa mara ya kwanza.

Hata hivyo mashabiki wanahofia shindano jingine kufanyika katika eneo hilo kutokana na mtikisiko mkubwa wa mashindano kipindi cha majira ya baridi.

Shabiki mmoja alisema; "Mashindano mengine yatafanyika kipindi cha baridi? huu mzaha kweli."

Mwigine akaandika; "Mashindani mengine ya Kombe la Dunia kipindi cha baridi? majanga."

Shabiki wa tatu akasema; " Kombe la Dunia kati kati ya msimu? hapana asanteni."

Wakati huo huo Uturuki imejiondoa katika kinyanganyiro cha kuwania uenyeji wa fainali za Euro mwaka 2028 ikiwapa nafasi Uingereza ambayo itawakilishwa na mataifa matano (Wales, Scotland, Ireland ya Kaskazini).

Chanzo: Mwanaspoti