Shirika kubwa la habari mashariki ya kati Saudi Media Group wametoa ofa ya £2.7 billion kutaka kununua klabu inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza klabu ya Chelsea.
Klabu ya Chelsea kwa sasa wana hali ngumu ya kutaka kuhakikisha wanaweza kupata bajeti ya kutosha kutokana na serikali kuwapa ukomo wa matumizi wa kulingana na vikwazo waliyowekewa.
Mpaka sasa klabu ya Chelsea kuna kuna wanunuzi 20 ambao wameonesha nia lakini mchakato huo unaendelea kwenye ngazi ya serikali na kampuni hizo huku Saudi Media Group inaongeza namba ya kuwa kampuni ya 21 kuweka offa ya kuhitaji klabu hiyo.
Saudi Media Group wanakadiliwa kutengeneza kiasi cha £770million kwa mwaka wakati mnunuzi yeyote anayetokea nchini saudi arabia iwe kampini ya kushirikiana au kampini binafsi haipaswi kuwa na uhusiano wowote na serikali ya nchi hiyoi.
Saudi Media Group baada ya kuweka ofa ya kununua klabu hiyo wameweka vipaombele vyao ambavyo ni kuuboresha uwanja wa Stamford Bridge, na akademi ya klabu kwenye uwanja wa mazoezi Cobham pia timu ya wanawake kuifanyia maboresho zaidi.