Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saudi Arabia wazidi kukomaa na Becker hadi kieleweke

Allisson Becker Injury Alisson Becker, 31

Wed, 5 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Matajiri kutoka Saudi Arabia bado wanapambana kuhakikisha kipa wa Liverpool, Alisson Becker anatua katika kikosi chao msimu ujao.

Becker amekuwa akitajwa kuondoka Liverpool tangu mwezi uliopita ikielezwa anataka kufanya hivyo ili kupata changamoto mpya na hapo ndipo matajiri hao wa Saudia walipopata fursa ya kuanza kuiwania saini yake.

Taarifa kutoka Teamtalk zinaeleza moja ya sababu zinazomfanya Becker ahitaji ni kuondoka kwa kocha Jurgen Klopp ambaye anaenda kupumzika baada ya kufanya kazi hiyo kwa misimu tisa akiwa Anfield.

Inaelezwa matajiri hao wa Saudia wanataka kumpa kipa huyu mshahara wa zaidi ya Pauni 400,000 kwa wiki kiasi ambacho inaonekana kuwani ngumu kwake kukikataa, licha ya mkataba wake kuwa unamalizika mwaka 2027.

Liverpool ipo tayari kumwachia katika dirisha hili ikiwa itapokea ofa nzuri na inafanya hivyo ili kupata pesa kwa ajili ya kushusha nyota wapya.

Msimu uliomalizika alicheza mechi 32 za michuano yote na kufungwa mabao 32, huku mechi 11 akimaliza bila ya kuruhusu nyavu zake kutikisika.

Liverpool huenda ikahitaji zaidi ya Pauni 50 milioni ili kumwachia fundi huyu wa kimataifa wa Brazil.

REAL Madrid imeanza mchakato wa kumsainisha mkataba wa kudumu mshambuliaji wa Espanyol anayecheza kwa mkopo katika timu yao Joselu, 34. Mabosi wa Madrid wanataka kumsainisha mkataba wa kudumu staa huyu kwa sababu wamevutiwa na kiwango alichoonyesha katika michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu uliomalizika na alifunga mabao mawili mchezo wa nusu fainali dhidi ya Bayern Munich.

ARSENAL haina mpango wa kumuuza straika wao Eddie Nketiah, 25, dirisha lijalo la majira ya kiangazi licha ya utitiri wa timu zilizo tayari kutoa pesa kwa ajili ya kuipata saini yake. Taarifa kutoka The Sun zinaeleza Fulham inataka kutoa Pauni 30 milioni kwa ajili ya staa huyu. Mbali ya Fulham staa huyu raia wa England huduma yake pia inahitajika na Crystal Palace, Wolves na Everton.

ARSENAL ipo tayari kusikiliza ofa kutoka timu mbalimbali zitakazohitaji huduma ya beki wao wa pembeni Oleksandr Zinchenko, 27, dirisha lijalo la majira ya kiangazi kwa sababu haonekani tena kuwa katika mipango ya Mikel Arteta kwa msimu ujao. Mara kadhaa staa huyu wa kimataifa wa Ukraine amekuwa akihusisha na Bayern Munich.

LIVERPOOL inataka kutoa Pauni 30 milioni kwenda Leeds United kwa ajili ya kumsajili winga wa timu hiyo raia wa Uholanzi, Crysencio Summerville katika dirisha hili. Summerville ambaye mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2026. Msimu uliomalizika amecheza mechi 49 za michuano yote na kufunga mabao 21. Liverpool inataka kujiimarisha eneo la kiungo ambalo msimu uliopita lilipwaya.

MABOSI wa Sunderland hawahitaji kumuuza kiungo wao raia wa England, Jobe Bellingham, 18, katika dirisha hili licha ya Tottenham, Brentford na Crystal Palace zote kuonyesha nia ya kutaka kumsajili. Jobe ambaye ni mdogo wake Jude Bellingham, mwenyewe anahitaji kuondoka kujiunga na timu itakayomfanya aonekane zaidi ya sasa.

MANCHESTER United na Liverpool zinamfuatilia kwa karibu beki wa kati wa Sporting Lisbon, Goncalo Inacio, 22, wanayehitaji kumsajili dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Goncalo ni mmoja wa mabeki wa kati waliofanya vizuri kwa mwaka huu Ureno kiasi cha kuvutia vigogo wengi barani Ulaya. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2027.

ASTON Villa ipo kwenye hatua za mwisho kukamilisha uhamisho wa kiungo wa Luton Town, Ross Barkley dirisha hili kwenye dili litakalowagharimu Pauni 5 milioni. Barkley aliyekuwa akihusishwa na Man United katika siku za hivi karibuni. Msimu uliomalizika alicheza mechi 37 za michuano yote na kufunga mabao mtano.

Chanzo: Mwanaspoti