Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saudi Arabia warudi tena kuivuruga Ulaya

Skysports Liverpool Manchester City Mohamed Salah Kevin De Bruyne Premier League 4202484 Saudi Arabia warudi tena kuivuruga Ulaya

Fri, 24 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dirisha la usajili la majira ya kiangazi limekaribia na Ligi Kuu ya Saudia huenda ikawekwa rekodi nyingine ya kusajili nyota wakubwa barani Ulaya kwa pesa ndefu.

Kwa mujibu wa ripoti Al Hilal ya Saudia huenda ikatoa zaidi ya Euro 175 milioni kwa ajili ya kumchukua mshambuliaji wa AC Milan Rafael Leao usajili ambao utavunja rekodi kwa kuwa ghali zaidi.

Katika dirisha la majira ya kiangazi mwaka jana Ligi Kuu Saudia ilitumia Pauni 701 milioni kutoka Pauni 5.9 bilioni zilizotumiwa na timu zote ulimwengu.

Wachezaji kama Neymar, Karim Benzema, N’Golo Kante, Sadio Mane, Riyad Mahrez na Ruben Neves wote walichukuliwa.

Inaelezwa, msimu huu Leao na wachezaji wengine wa England kama Alisson Becker, Kevin De Bruyne na Mohamed Salah wanaweza kutua nchini humo kwa gharama kubwa.

Timu kadhaa za England zimewahi kuhusishwa na Leao lakini sasa Wasaudia wamepanga kupindua mezani na kumchukua kwa dau hilo nono.

Katika taarifa iliyoripotiwa na tovuti ya Sportsbibble, baba yake Leao anatarajiwa kusafiri hadi Saudia wiki hii kwa ajili ya mazungumzo na Al Hilal juu ya uhamisho wa mtoto wake.

Al Hilal ambayo ndio bingwa wa msimu uliomalizika wa Ligi Kuu Saudia, inataka kuboresha kikosi chao ili kufanya vizuri katika fainali za Kombe la Dunia la Vilabu la 2025 ambapo wanaweza kumenyana na Manchester City na Chelsea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live