Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Saudi Arabia kuwania kuandaa fainali za Kombe la Dunia 2034

Kombeeee Saudi Arabia yatangaza kuwania kuandaa Kombe la Dunia 2034

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Saudi Arabia imetangaza rasmi mpango wake wa kuwania kuandaa kombe la Dunia la FIFA 2034 katika kampeni ya kugeuza ufalme huo kuwa na nguvu kwenye tasnia ya michezo kimataifa.

Hatua hiyo la Saudia imekuja muda mfupi baada ya Shirikisho la soka Duniani FIFA kuthibitisha Uhispania, Ureno, Morocco, Paraguay, Argentina na Uruguay kwa pamoja zitakuwa wenyeji wa kombe la Dunia 2030 huku ikizialika nchi za Shirikisho la Soka la Asia kuwasilisha zabuni kwa 2034.

Katika taarifa yake Waziri wa Michezo wa Saudia Prince Abdulaziz bin Turki Al Faisal amesema: “Kuandaa Kombe la Dunia la FIFA mwaka 2034 kutatusaidia kufikia ndoto yetu ya kuwa taifa linaloongoza katika michezo ya dunia na itakuwa hatua muhimu katika mageuzi ya nchi.”

Saudi Arabia imefuzu Kombe la Dunia, mara sita kihistoria huku mwaka 1994 ukiwa mwaka wao wa kwanza kushiriki. Mnamo 2022 Saudi Arabia iliwaduwaza wadau wa soka Duniani baada ya kuwafunga Argentina (2-1) ambao ndio walikuwa Mabingwa wa michuano hiyo huko Qatar.

Habari hizi pia zinakuja wakati ambapo ligi ya Saudia Pro League ikijivunia kuwa na vipaji bora zaidi duniani kufuatia ujio wa wakali wa soka kama Cristiano Ronaldo, Neymar na Karim Benzema waliohamia kwenye kucheza kwenye ligi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live