Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sassoulo yaweka rekodi dhidi ya Juventus

0 GettyImages 1341315698 Nyota wa Juventus, Paulo Dyabala (Kulia ) na Manuel Locatelli (Kushoto)

Thu, 28 Oct 2021 Chanzo: eatv.tv

Massimiliano Allegri amekuwa kocha wa tatu kuingoza Juventus katika mechi 200 kwenye Serie A baada ya Giovanni Trapattoni na Marcelo Lippi pamoja na rekodi hiyo Allegri alijikuta akikumbana na kipigo cha bao 2-1 katika uwanja wake wa nyumbani kutoka kwa Sassoulo.

Wakati Juventus wakikutana na kipigo hicho, lakini iliwekwa rekodi kwa Sassoulo ambao walipata ushindi wao wa kwanza dhidi ya Juventus baada ya kufanya majaribio mara 9 bila kufanikiwa.

Mabao yaliyopelekea Juventus kupoteza mechi hiyo yalifungwa na Davide Frattesi na Mattia Perin na kuipa ushindi muhimu Sassoulo wakiwa ugenini huku bao la wenyeji likiweka kambani na Paulo Dyabala.

Kipigo hicho ni cha tatu kwa Juventus katika Ligi Kuu ya Italia msimu huu na ni kwa mara ya kwanza tangu 1996 kibibi kizee cha Turin kinapoteza mechi tatu kati ya kumi za mwanzo katika Serie A, kuwaacha alama 13 nyuma ya vinara AC Milan wenye alama 28.

Nao mabingwa watetezi wa Ligi hiyo, Inter Milan waliibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Empoli, mabao yaliyofungwa na Danilo D'Ambrosio na Federico Dimarso na kuimarisha nafasi ya tatu katika msimamo wakiwa na alama 21.

AS Roma walifanikiwa kupata ushindi wao wa kwanza baada ya mechi tatu, walipotokea nyuma dhidi ya Cagriali na kushinda bao 2-1 na sasa wamechupa hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa Serie A wakiwa na alama 19.

Matokeo mengine ni kwamba Atalanta iliinyuka Sampdoria bao 3-1,Udinese na Hellas Verona walitoka sare ya bao moja,nayo Lazio iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Fiorentina. 

Chanzo: eatv.tv