Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sasii akabidhiwa filimbi Yanga vs Simba

Saaaaaasiii Elly Sasii

Fri, 12 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwamuzi Elly Sasii anatarajia kuwa mwamuzi wa kati kwenye mchezo wa dabi ya Kariakoo kati ya Yanga dhidi ya Simba utakaochezwa Agosti 13, Uwanja wa Mkapa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi Tanzania iliweka wazi kuwa kwenye mchezo huo jumla ya waamuzi ambao watatumika ni watano mmoja kati wawili wasaidizi namba moja na namba mbili huku wawili wakiwa ni mwamuzi wa akiba na mtathimini waamuzi ambaye ni Nassor Hamdun (Kigoma).

Taarifa zinaeleza kuwa Sasii atakuwa kati wakati Mohammed Mkono kutoka Tanga atakuwa mwamuzi msaidizi namba moja na Kassi Mpango kutoka Dar es Salaam atakuwa mwamuzi msaidizi namba mbili.

Taarifa hiyo iliweka wazi jina la mwamuzi wa wa akiba kwenye mchezo huo kuwa ni Ramadhan Kayoko (Dar es Salaam).

Mchezo huo ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku huo utakuwa ni mchezo wa nane kwa timu hizo kukutana tangu Ngao ya Jamii ilipoasisiwa mwaka 2001 Simba ikichukua mara nne, Yanga mara tatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live