Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sasa ni wakati wa kuonyesha viwanjani

Benchikha X Gamondi Kimataifa Sasa ni wakati wa kuonyesha viwanjani

Wed, 7 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Ligi Kuu imerejea baada ya mapumziko ya zaidi ya mwezi mmoja kupisha michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2023) inayopigwa Ivory Coast

Kutokana na mapumziko, timu zilipata fursa ya kujifua ili kujiandaa na mikikimikiki hiyo mara itakaporejea ili kuendelea pale zilipoishia na ni matumani yetu kwamba baada ya takriban mechi nne zilizozihusisha Simba na Yanga, kila timu imeshajipanga namna gani itakavyoanza masiha mapya.

Pamoja na maandalizi ya kiufundi, kimbinu na kimikakati, lakini ni vyema wachezaji baada ya kujitathmini katika namna ambayo walitumia fursa ya mapumziko kufanyia kazi kipengele cha kupunguza makosa uwanjani na pia kuziwezesha timu zao kushinda mechi, hivyo ni wakati wa kila timu kupambana hivi sasa.

Tunapozungumzia makosa uwanjani, hii imekuwa ni changamoto kubwa miongoni mwa timu hizo kiasi kwamba huzinufaisha kiaina timu pinzani ambazo zinapambana nazo katika michezo mbalimbali ya ligi hiyo na katika mashindano mengine ikiwamo yale ya kimataifa kwa zile zinazoshiriki. Yapo makosa ya kiufundi kwa maana ya yale yanayotokea kwa kushindwa kufanyia kazi mbinu, lakini kuna makosa ya kinidhamu ambayo ni kushindwa kujichunga kitabia kwa mchezaji au timu nzima ili kuepukana na adhabu ya vipigo kutoka kwa timu pinzani.

Mfano wa makosa ya kinidhamu ni kukosa heshima kwa waamuzi na wachezaji wa timu pinzani ambapo kuna baadhi ya wachezaji wamekuwa wakitumia lugha chafu kwa waamuziz na kwa wenzao wakiona hiyo ni njia ya kuwatoa mchezoni kisaikolojia.

Lakini pia wengine wamekuwa wakicheza rafu za makusudi tena katika mazingira ambayo yanakuwa hayana ulazima kwao kufanya hivyo wakiamini kwamba inasaidia kupunguza ubora wa wapinzani na kuwapa hofu. Mwisho wa siku makosa hayo huchangia baadhi kuonyeshwa kadi ama za njano au nyekundu au kusababisha adhabu za faulo ama penalti ambazo baadhi huzipa mabao timu pinzani. Kwa makosa ya kimbinu yako mengi mfano ni wachezaji kushindwa kuwa katika maeneo sahihi kulingana na nafasi zao katika nyakati muhimu wakati wa mchezo ambazo ni pindi timu inaposhambulia au inaposhambuliwa na wakati ina mpira au inapokuwa haina mpira.

Kwa upande wa makipa wamekuwa na changamoto kubwa katika kutimiza majukumu muhimu ya nafasi yao kama vile kuondoa hatari zitokanazo na mipira ya krosi, kukamata mipira kwa usahihi na mikono, lakini pia kuzipanga safu zao za ulinzi.

Jambo jingine ambalo tunaamini kwamba linapaswa kuendelea kuwekwa sawa wakati huu ligi ikirejea ni utunzaji wa maeneo ya kuchezea katika viwanja jambo ambalo linafanya mpira uchezeke vyema na hata muonekano mbele ya macho ya watazamaji kuwa wa kuvutia.

Haimaanishi kwamba hakuna viwanja ambavyo maeneo ya kuchezea hayako vizuri, vipo lakini namba yake ni ndogo kulinganisha na vile ambavyo vimetunzwa na vina ubora mzuri. Hivyo hayo yote ni muhimu yakazingatiwa na kuhakikisha kwamba yanalindwa wakati huu ligi ikirejea.

Chanzo: Mwanaspoti