Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sarpong, Lamine wazua hofu Yanga

Zoezi Pic Data Sarpong, Lamine wazua hofu Yanga

Thu, 15 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Wachezaji nyota wa Yanga, Saido Ntibazonkiza, Lamine Moro na Michael Sarpong wamezua hofu baada ya kutoonekana katika mazoezi yaliyofanyika juzi Jumanne asubuhi.

Mwanaspoti lililokuwa uwanjani hapo lilishuhudia nyota hao wakikosekana wakati wa programu ya kaimu kocha mkuu, Juma Mwambusi ikiendelea.

Saido na Moro walikuwa katika kikosi kilichocheza mchezo wa ligi dhidi ya KMC uliomalizika kwa sare 1-1.

Wakati nyota hao wakikosekana, Kocha wa makipa Razak Siwa na makipa wake Farouk Shikhalo na Ramadhan Kabwili wao waligeukia katika fukwe za bahari kwa ajili ya kujiweka sawa wakijiandaa na mechi zijazo za ligi.

Katika mazoezi hayo Mwambusi alikuwa anaangalia zaidi kumiliki mpira kitu kilichokosekana katika mchezo wao uliopita uliowafanya mabosi wa Yanga kufikiria kumleta fasta nchini, Sebastian Migne kuongeza mzuka kambini.

Mwambusi alitumia makundi matatu ya wachezaji aliokuwa amewapanga na kuwataka wacheze kwa pasi za haraka haraka. Baada ya zoezi hilo kuonekana kueleweka, alibadilisha zoezi na kuwaambia wacheze kwa kugusa mpira mara moja na kuachia huku wakipeana nafasi.

Wachezaji walitumia saa moja na nusu baada ya kuanza saa 2:30 na kumaliza saa 4:00. Wachezaji waliokuwepo katika mazoezi ni Haruna Niyonzima, Said Makapu, Wazir Junior, Tonombe Mukoko,Fiston Abdulrazack, Kibwana Shomari, Yacouba Sogne, Paul Godfrey ‘boxer’, Feisal Salum. Wengine ni Adeyum Saleh, Zawadi Mauya, Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Deus Kaseke, Abdallah Shaibu, Carlos Carlinhos, Ditram Nchimbi, Farid Mussa na Tuisila Kisinda. Yanga mechi ijayo inacheza na Biashara United kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz