Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sare ya Tabora United yamweka Kocha Azam FC matatani (+Video)

Dabo Kocha Azam Sare ya Tabora United yamweka Kocha Azam FC matatani

Tue, 20 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Jana Azam FC kulazimisha sare ya bila kufungana na Timu ya Tabora United ya Mkoani Tabora.

Mchambuzi wa Michezo kutoka E-Fm, Jemedari Said ameandika;

Video ya kwanza Kocha Yusuf Dabo na baadhi ya wachezaji wake wakizungumza na mwamuzi katika namna ya kutofurahishwa na jambo mara baada ya mchezo kumalizika.

Video namba 2 Kocha Yusuf Dabo akihoji kwanini ligi ya Tanzania ambayo ni moja ya ligi bora Afrika ilikosa mwamuzi kwenye AFCON? Akaongeza kusema kama tunataka kuendeleza mpira waamuzi wanabidi wajipange.

Itategemea ripoti ya mwamuzi wa mchezo inasemaje kutokana na kile kilichoonekana kwenye video ya kwanza. Lakini Kamati itajielekezaje baada ya vitendo vya kwenye video ya kwanza na maelezo ya kwenye video ya pili, kama itaangukia kwenye kanuni ya 45 Udhibiti wa makocha kifungu cha 2:1 na 2:2. Lakini pia wachezaji kwenye video ya kwanza si ajabu kukitokea wa kuingia kwenye janga kutokana pia na ripoti ya mwamuzi na kamati itakavyojielekeza, ikibainika vinginevyo başı kanuni ya 41-5(5:3) inaweza kumzoa yeyote mwenye bahati mbaya. Wacha tusubiri tuone

View this post on Instagram

A post shared by Jemedari Said Kazumari (@jemedarisaid)

Chanzo: www.tanzaniaweb.live